
Mlinda lango alifanikiwa kujitetea/Hisani
Klabu ya PSV imempiga marufu ya miaka 40 shabiki matata aliyeingia uwanjani na kumvamia mlinda lango wa Sevilla, Marko Dmitrovic.
Shabiki huyo mwenye umri wa miaka 20 alimfumania Dmitrovic, 31, baada ya timu yake kushindwa 2-0 katika mechi ya Ligi ya Uropa mnamo Februari 23, 2023.
“Sikutarajia hayo, nilivamiwa ghafla usoni ila sikuumia,” alisema mlinda lango huyo kutoka taifa la Serbia.
Shabiki huyo, kando na kupigwa marufuku kuingia uga wa Philip’s, pia amefungwa miezi mitatu gerezani.
Shirikisho la Michezo Uropa pia linatarajiwa kutoa uamuzi kutokana na tukio hilo.
PSV, kupitia tovuti yake, imesema mikakati imewekwa kuhakikisha jambo kama hilo halifanyiki tena.

Tom Lutali thrives in covering and writing sports fashionably in Kiswahili, a language he has mastered in telling stories in the most elaborate way. A graduate of media studies at the Elgon View College, Tom is a shining star in the media industry.