Ni rasmi kwamba, Wajukuu wa Pharaoh wamefuzu katika hatua ya nne bora baada ya kuwafunga Morocco 2-1.
Morocco, walianza mechi hiyo kwa kishindo na dakika ya saba, wakapata penalti kisha Boufal akawapa Simba hao wa jangwani uongozi wa mapema.
Kipindi cha kwanza kiliisha Morocco wakiwa kifua mbele 1-0. Kipindi cha pili, wajukuu hao wa Pharaoh walikuja kwa kishindo ndipo mshambulizi wa Liverpool Muhammad Salah, akiregesha bao hilo dakika ya ’52.
Mechi hiyo iliisha muda wa kawaida 1-1 na ikaenda muda wa ziada ndipo Trezequet akafungia Misri bao la pili na la ushindi dakika ya ‘100. Kwa sasa, Misri watakutana na wenyeji Cameroon Alhamisi ijayo katika nusu fainali. Kisha mshindi atatinga fainali.
Kwingineko, Senagal walijikatia tiketi ya nusu fainali baada ya kuwaadhibu Limbukeni Equatorial Guinea 3-1. Mabao kutoka kwa Famara Diedhiou, Bouna Sarr na Pepe Kouyate, yaliivukisha Senagal nusu fainali ambapo itakutana na Burkina Faso jumatano. Bao la pekee la Equatorial Guinea, lilifungwa na Buyla.
Kwa sasa, Kipute hicho kinachukuwa mapumziko ya siku mbili kisha kurejelewa jumatano.
Jumatano tarehe 2, Februari 2022
Burkina Faso vs Senagal – 10:00pm
Alhamisi, Februari 3, 2022
Cameroon vs Eggypt – 10:00pm
Imehaririwa na Ian Elroy Ogonji

Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.