Shabiki sugu wa timu ya taifa Harambee Stars na AFC Leopards (Ingwe), Isaac Juma, amepumzishwa nyumbani kwake Mumias, kaunti ya Kakamega.
Juma aliuwa majumaa mawili yaliyopita kutokana na mzozo wa ardhi baada ya kuvamiwa na genge la wahuni waliokuwa wamejihami kwa silaha.
Waombolezaji walionyesha huzuni kwa kuvalia nguo zenye nembo ya Kenya na kujichora jinsi mwendazake alikuwa akifanya wakati wa mechi za Ingwe na Stars.
Kulikuwa pia na viongozi mashuhuri akiwemo gavana wa Kakamega Wycliffe Opranya.
Kwenye mazishi hayo, swala la mzozo wa shamba lilitamalaki huku ndugu, jamaa na marafiki wakiomba serikali ya kaunti na ile ya kitaifa kuingilia kati ili kusuluhisha swala hilo.
Brian Juma, mwanawe mwendazake amesema hawataishi kamwe katika shamba hilo kutokana na kuhofia maisha yao.
“Babangu wakati alikuwa akija nyumbani baada ya mechi, alikuwa akituambia dadake hakuwa akimpa lepe la usingizi kutokana na swala la ardhi. Tafadhali serikali, amkeni na mtuambie wapi tutaenda. Hatuwezi ishi kwa hili shamba ,” alisema.
Mwendazake amewaacha watoto 15 na wajane wawili.

Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.