- Na Dennis Avokoywa
Wazee wa jamii ya Abaluhya leo wamemfanyia tambiko fahali aliyemgonga na kumuua mwanamume wa miaka 40 katika eneo bunge la Mumias Mashariki, kaunti ya Kakamega.
Joseph Opanda alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakifanya matayarisho ya mashindao ya mafahali iliyoratibiwa Disemba 26.
Fahali huyo wa thamani ya Sh 95,000 alinunuliwa wiki iliyopita na kakake marehemu.
Ad

Kidesturi, mara tu baada ya fahali kumgonga na kumuua mmiliki au shabiki wakati wa shindano, yeye hukatakatwa akiwa hai kisha nyama yake hushindaniwa na mashabiki bila vikwazo vyovyote.
Utamaduni huu hufanywa baada ya fahali kumgonga na kumuua shabiki au mmiliki na inaaminika huwa inakinga wanafamilia waliyosalia dhidi ya mapepo ya mwendazake. Pia huzuia kisa kama hicho kujirudia.