Wezi wavunja baa na kuiba pombe Vihiga
Mlango wa baa uliovunjwa Vihiga [Picha-Hisani]

Wezi wavunja baa na kuiba pombe Vihiga

Wezi hao pia waliiba mali nyingine.

Watu wasiojulikana wamebomoa baa na duka katika soko la Lotego, kaunti ya Vihiga, na kutoroka na pombe pamoja na mali ya thamani ya maelfu ya pesa usiku wa kuamkia leo.

Kulingana na mwathiriwa hiyo Geoffrey Agufa, alipigwa na butwaa alipopata mlango wa baa yake uko wazi na umebolewa, runinga na redio yake vimeibiwa.

Paa ya baa baada ya wezi kutoweka na mali [Picha-Hisani]

“Nilipofika hapa, nilishtuka sana kupata mlango umebolewa na uko wazi kuingia ndani, hakuna kitu. Pombe imeibiwa,” alisema.

Wezi hao pia walivunja duka lake na kuiba shilingi elfu tano na mafuta ya kupikia.

Bwana agufa ametoa wito kwa idara ya usalama eneo hilo kuharakisha uchunguzi ili apate haki.

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *