Familia moja Molem katika eneo bunge la Endebess, kaunti ya Trans Nzoia, inalilia haki baada ya mwanao mwenye umri wa miaka 21 kuuawa kinyama katika shamba la mahindi na watu wasiojulikana.
Rose Simiyu, mamake msichana huyo amesema kuwa mwanawe alikuwa akiwatafutia ng’ombe nyasi wakati alipotendewa unyama huo.
“Mtoto wangu wamemgonga vibaya wamemvunja shingo, naomba serikali inisaidie mtoto wangu nipate haki,” mama Rose alilalama.
Kulingana na wakazi, visa vya mauaji vimekithiri eneo hilo huku wakitaka idara za usalama kushika doria.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.