- Na BBC
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameshtumu matamshi yaliyotolewa na mwenzake wa Marekani Joe Biden kuhusu ‘uvamizi’ mdogo wa Urusi katika taifa lake.
Bwana Biden alikuwa amependekeza kwamba uvamizi mdogo huenda ukavutia majibu ya kiwango kama hicho kutoka kwa Marekani na washirika wake. Lakini bwana Zelensky alituma ujumbe wa Twitter akisema: “Hakuna uvamizi mdogo, sawa na kwamba hakuna majeruhi madogo na huzuni ndogo kutokana na kupoteza wapendwa”.
Urusi ina takriban wanajeshi 100,000 karibu na mpaka lakini inakanusha kupanga uvamizi
Rais Vladmir Putin ametoa masharti, akisisitiza kuwa Ukraine haipaswi kamwe kuruhusiwa kujiunga na Nato na kwamba muungano huo wa kujihami unapaswa kuacha shughuli za kijeshi mashariki mwa Ulaya.
Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.