
Kenya Administration Police vehicle [Photo-Courtesy]
Wenyeji wa kijiji cha Vilobgo cha wadi ya Mautuma katika kaunti ndogo ya Lugari, Kakamega, wameachwa vinywa wazi baada ya mama kumpiga mwanawe wa miaka 10 hadi kufariki.
Chifu wa kata ya Mautuma Bi Pamela Davava Kulali aliambia West FM kuwa Melvin Awinja, ambaye ni mwanafunzi wa Gredi ya Pili katika shule ya msingi ya Mahiga, sababu ya mamake kumpiga bado haijabainika.
Bi Pamela aliongezea kuwa baada ya mamake kugundua kwamba mwanawe alikuwa amezidiwa baada ya kichapo, aliamua kumkimbiza katika hospitali ndogo ya Mautuma na hapo ikadhibitishwa kuwa ameaga dunia.
Bi Pamela aliongezea kuwa baada ya familia ya mwendazake kugundua amefariki ilianza mikakati kisiri ila chifu huyo aligundua mapema na kuripoti katika kituo cha polisi cha Mlimani.
Mwili wa msichana huyo uliondolewa na maafisa wa polisi wa Turbo na unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya Kimbilio iliyoko kaunti jirani ya Uasin Gishu huku uchunguzi ukianzishwa.

Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.