Watu watatu waliaga dunia Ijumaa mchana baada ya trela kukosa mwelekeo na kubiringika katika eneo la Lwandeti kwenye barabara kuu ya Eldoret-Webuye.
Walioshuhudia ajali hiyo wanasema dereva wa trela hilo alipoona limemshinda kudhibiti aliruka nje.
Trela hiyo iliyokuwa ikisafirisha vifaa vya ujenzi kutoka pwani ya Kenya na kuelekea nchi jirani ya Uganda linadaiwa kupoteza mwelekeo huku likigonga na kumjeruhi vibaya mhudumu wa bodabda kabla ya kuanguka na kuwauwa makanga wawili papo hapo.
Ajali hii ni ya tatu chini ya mwezi mmoja katika barabara hiyo.
Miili ya wafu iliondolewa na maafisa wa kituo cha polisi cha Webuye na inahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya Webuye.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.