Ndivisi: Kijana wa kidato cha kwanza ajitoa uhai kwa kukataliwa na mpenziwe wa kidato cha nne
[Picha-Hisani]

Ndivisi: Kijana wa kidato cha kwanza ajitoa uhai kwa kukataliwa na mpenziwe wa kidato cha nne

Mauti: Wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi tangu shule ya msingi.

Wingu jeusi limetanda katika kijiji cha Lutacho, wadi ya Ndivisi, eneo bunge la Webuye Mashariki katika kaunti ya Bungoma baada ya mwanafunzi wa kidato cha kwanza kunywa sumu na kufariki kutokana na mzozo wa kimapenzi.

Willy Juma, mwendazake, inasemekana amekuwa katika uhusiano na mwanafunzi wa kike wa kidato cha nne katika shule ya upili ya Lutacho tangu wakiwa shule ya msingi kabla ya mapenzi yao kuanza kuyumbayumba hivi karibuni.

“Uhusiano wao umekuwa dhabiti na hata huyo msichana alikuwa akiamka mapema saa kumi usiku akienda kwa akina kijana kisha anatoka saa kumi na mbili asubuhi akienda shule,” alisema Ezekiel Lusweti, jiraniye kijana huyo.

Inasemekana baada ya kijana huyo kukataliwa, aliamua kunywa sumu kabla ya kukimbizwa katika hospitali kuu ya Webuye alipokata roho.

Chifu wa eneo hilo Bwana Samwuel Nayombe amewarai vijana wasisukumwe na vitu vidogo ambavyo vinaweza kuwaletea madhara kama hayo.

“Vijana, hasa wale ambao wangali shuleni, someni kwanza na mambo mengine yatakuja baadaye,” alifoka Bwana Nayombe.

Mwili wa mwendazake unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya Webuye, kaunti ya Bungoma, huku maandalizi ya mazishi yake yakianza.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *