Mlima Elgon: Mwanamume apigwa na kufariki kwa madai ya kumuua mkewe
Kenya Administration Police vehicle [Photo-Courtesy]

Mlima Elgon: Mwanamume apigwa na kufariki kwa madai ya kumuua mkewe

Kwa mukhtasari: Mwanamume huyo anasemekana kumvamia mkewe kwa upanga.

Biwi la simanzi limetanda Mlima Elgon, kaunti ya Bungoma, baada ya mwanamume kupigwa na umma kwa madai ya kumuua mkewe kinyama.

Mark Karani anasemekana kumkatakata mkewe Cristabella Karani, mwalimu wa shule moja ya msingi eneo hilo, baada ya wawili hao kugombana Jumanne usiku nyumbani kwao.

Bi Karani alipiga mayowe yaliyowavutia majirani ambao walifurika nyumbani kwake na kumpata anavuja damu kabla ya kukata roho.

Bwana Karani aliaga dunia baada ya kufikishwa katika zahanati ya Cheptais ambako alikuwa amekimbizwa na maafisa wa polisi waliokuja kumnusuru kutoka kwa wananchi waliokuwa na ghadhabu.

Kamishna wa kaunti ya Bungoma Samwuel Kimiti alisema polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na chanzo cha tofauti kati ya wawili hao. Makachero kutoka Eldoret pia wameanza uchunguzi kuhusiana na kisa hicho cha kusikitisha.

Miili hiyo yote inahifadhiwa katika hifadhi ya maiti Bungoma.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *