Kimilili: Mwanamume aliyenusurika pombe ya sumu afariki baada ya kuibugia tena
Pombe haramu ikimwagwa [Picha-Hisani]

Kimilili: Mwanamume aliyenusurika pombe ya sumu afariki baada ya kuibugia tena

Mwanaume huyo alinusurika hapo awali

Wingu jeusi limetanda katika kijiji cha Kananai, eneo bunge la Kimilili, Bungoma, baada ya mwanamume mmoja kuaga dunia baada ya kunywa pombe ya sumu almaarufu chang’aa siku tu chache baada ya kunusurika.

Eugene Wafula, 33, aliaga dunia baada ya kunywa kileo hicho kilichoharamishwa kutoka katika kituo kimoja ambapo watu watano waliaga dunia Jumatano.

Wafula na wenzake takribani 12 walikimbizwa katika hospitali ndogo ya Kimilili baada ya kulalamikia maumivu ya tumbo na udhaifu wa mwili mzima.

Wafula alikuwa miongoni mwa wale walioepuka kifo na wakatibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani Alhamisi huku wenzake watano wakiangamia.

Ila uraibu wake ulimuelekeza kuko huko na akaagiza glasi nyingine na muda si muda alianza kuhisi maumivu ya tumbo na akakimbizwa katika hospitali ndogo ya Kimilili Ijumaa jioni, ila wakati huu hakuwa na bahati.

Polisi, madakatari na wataalamu wameanzisha uchunguzi kubaini kemikali inayotumika kuunda pombe hiyo.

Wenyeji sasa wanatoa wito kwa idara husika kuajibika kikamilifu kuhusiana na swala hilo.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *