Liverpool imefululiza ushindi wao dhidi ya Villarreal baada ya kuwabomoa mabao 3-2 katika ngarange ya Ligi ya Mabingwa Ulaya raundi ya pili katika nusu fainali ugani Estadio de la Ceramica.
Villarreal waliuanza mchezo kwa kujituma na kuishia kuwafunga Liverpool mabao mawili dakika ya 3 na 41; Boulaye Dia na Francis Coquelin wakifunga kila mmoja mtawalia.
Kipindi cha pili, Wekundu walijikakamua na nguvu sawa na Villarreal kwa umilisi wa mpira. Kunako dakika ya 62, pasi kutoka kwa Mohamed Salah ikatiliwa katika guu la kulia la Fabinho na kutia nyavuni. Dakika 12 baadaye, Sadio Mane akifunga goli la pili baada ya Navi Keita kumuundia pasi katika guu lake la kushoto.
Liverpool sasa inasubiri mshindi wa mechi kati ya Real Madrid na Manchester City inayotarajiwa kuchezwa usiku wa leo saa nne usiku baadaya kujikatia tiketi ya fainali.
Villarreal itapambana na atakayepigwa ili kupata nafasi ya tatu.
Discover the pulse of Western Kenya with WKT – your go-to digital media platform for real-time updates, rich perspectives, and powerful stories that matter.