Mama mmoja kutoka eneo bunge la Ikolomani, kaunti ya Kakamega, amepata baraka ya watoto wanne wa kiume baada ya kujifingua.
Alice Khasiala, 39, alijifungua pacha hao wanne kupitia njia ya upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Kakamega.
Khasiala amesema wakati alikuwa mjamzito hakufahamu amebeba pacha wanne mpaka pale ambapo alijifungua.
“Nilikuwa nikienda kliniki kama kawaida na sikuhisi kana kwamba nimebeba pacha wanne,” alisema mama huyo mwenye furaha.
Muuguzi mkuu wa hospitali hiyo, Patrisiana Nafula, amesema watoto hao wote ambao ni wa kiume wako buheri wa afya.
Kwa sasa mama huyo anaomba msaada wa wahisani kuwasaidia kuwalea watoto hao ikizingatiwa yuko na watoto wengine wa nne nyumbani.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.