Taharuki imetanda katika kijiji cha Makongeni eneo bunge la Nambale, Busia, baada ya msichana mmoja kuaga dunia na wengine watatu kuugua baada ya kula mihogo yenye sumu.
Watoto ambao walikimbizwa katika hospitali ya Nambale ni wa umri wa miaka mitano, sita na tisa.
Jamazaa zao wanasema watoto hao walianza kulalamikia maumivu ya tumbo na kutapika.
Wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Busia wamesema huenda walikula mihogo hiyo ikiwa mibichi ama kama imeoza.
“Walikula mihogo yenye sumu na ukiangalia hali yao si ya kawaida,” Daktari mkuu wa hospitali ya rufaa ya Busia, Dickens Etieng, alisema.
Wazazi wanetakiwa kuwa makini na vyakula ambavyo wanao wanakula.
Mwili wa mwendazake unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa ya Busia huku wale wengine watatu wakiendelea na matibabu.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.