
Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya [Picha-Hisani]
Wagombea viti vya uwakilishi wadi katika eneo bunge la Butere kupitia chama cha DAP-K wamemsuta vikali gavana wa Kakamega Wycliffe Ambetsa Oparanya kwa kile wanachokitaja kuwa njama ya kuwafungia nje ya uchaguzi mkuu ujao.
Wakiongozwa na Thomas Wanga wa Marama ya Kati, Edwin Anyanga wa Marama Magharibi na George Wasiche wa Marama Kusini, wagombea hao wamesema licha ya Oparanya kiongozi wa kampeni za Azimio eneo la Magharibi ameonyesha wazi kuwapendelea wapinzani wa chama chake cha ODM.
Viongozi hao wamesema kamwe hawatokubali ndoto zao kuzimwa na njama ya Oparanya kupitia mfumo wa muungano wa Azimio kutaka wagombea wenye nguvu zaidi kuachiwa nafasi.
Viongozi pia wamelalamikia kutohusishwa katika kampeni na mipangilio ya muungano wa Azimio na kusema iwapo wataendelea kutengwa hawatakua na budi kuwaunga mkono wagombea wa miungano mingine.
Hata hivyo, Oparanya na naibu mwenyekiti wa, DAP ambaye pia ni mbunge wa Lugari, Ayub Savula, wamejitenga na madai hayo wakiwataka wagombea hao kutumia muda wao kujipigia debe badala ya kuwalaumu.

Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.