Viongozi wa ANC wampongeza Ruto kwa kuzawadi viongozi wa Magharibi nyadhifa
David Wamatsi ambaye ameteuliwa na rais William Ruto kuongoza Bodi ya Utalii nchini/Hisani

Viongozi wa ANC wampongeza Ruto kwa kuzawadi viongozi wa Magharibi nyadhifa

Viongozi hao wameapa kusimama na Dr. Ruto

Viongozi wa chama cha Amani Nationa Congress (ANC) eneo bunge la Mumias Mashariki katika kaunti ya Kakamega wamempongeza rais William Ruto kwa kuendelea kuwateua viongozi kutoka eneo la Magharibi kushikilia nyadhifa mbalimbali za uongozi.

Wakiongozwa na Everlyne Makokha, viongozi hao wanasema hatua hiyo inaashiria kuwa rais William Ruto ni kiongozi anayeweza kuaminika na ambaye hutimiza ahadi zake.

“Kwa kweli, tuko na rais ambaye si msaliti, anatimiza alichosema katika kampeni zake,” alisema Bi. Makokha.

Wakiwahutubia wanahabari katika eneo la Shianda, viongozi hao walisisitiza kuwa eneo la Magharibi limenufaika pakubwa na serikali ya rais Ruto, wakimpongeza kwa kumteua aliyekuwa mgombea wa ubunge eneo hilo kwa tiketi ya chama cha ANC David Wamatsi kuwa mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Utalii.

Wameapa kuendelea kumuunga mkono Ruto ili kuhakikisha kuwa anawatimizia Wakenya ahadi alizowapa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu iliopita.

Wamemtaka rais Ruto kulipa kipao mbele swala la kukamilisha baadhi ya miradi iliyoanzishwa na rais mstaafu Uhuru Kenyatta na vilevile kufufua viwanda vilivyosambaratika.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *