
Polisi wamwaga pombe haramu/Hisani
Imebainika kuwa wauzaji wa pombe haramu katika eneo la Mlima Kenya sasa wanaendesha biashara hiyo katika maeneo chafu na yasiyofaa kama vile vyoo na makaburi.
Wagemaji hao wanatumia mbinu hiyo ili kukwepa kukamatwa na polisi wanaoendesha operesheni ya kumaliza biashara hiyo katika eneo hilo.
Operesheni hiyo iliamrishwa na naibu rais Rigathi Gachagua kumaliza pombe hiyo ambayo inawaathiti vijana na kupelekea kuvunjika kwa ndoa na familia.
Vijana katika kaunti za Nakuzu, Nyandarua, Nyeri na Laikipia wameathirika sana na ugemaji haramu.
Aidha, eneo la Magharibi limetajwa kama ngome ya biashara hiyo katika ripoti ya hivi majuzi.

Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.