Vijana wake Erik Ten Hag wanawakaribisha Chelsea ugani Old Trafford katika mechi ya Ligi Kuu nchini Uingereza leo saa nne usiku.
Man United watajikatia tiketi ya kuingia Champions League iwapo watashinda ama kutoka sare katika mechi hii.
Ushindi dhidi ya Chelsea utaimarisha kampeni yao ya kumaliza nafasi ya tatu mbele ya Newcastle ambao tayari wamefuzu Champions League.
Chelsea nao wanasaka kuboresha matumaini ya mashabiki wao baada ya msururu wa matokeo mabovu.
Katika mechi tano ambazo wamekutana, Mashetani Wekundu na Wanasamawi wametoa sare.
Mechi tatu zimeishia 1-1, mbili 0-0.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.