Elgeyo Marakwet: Taharuki baada ya wavamizi kutekeleza mauaji, kutoroka na mifugo 600
Picha [Maktaba-Hisani]

Elgeyo Marakwet: Taharuki baada ya wavamizi kutekeleza mauaji, kutoroka na mifugo 600

Taharuki imetanda katika kijiji cha Koitalia, Keiyo Kaskazini, baada ya wavamizi kuvamia wenyeji na kuua raia wawili na kujeruhi wengine saba kisha kutoroka na mifugo takribani 600.

Wezi hao walivalimia kijiji hicho mwendo wa saa saba mchana jana, kulingana na mwakilishi maalum wa Kaunti ya Elgeyo Marakwet Bi Winny Kanda.

“Rais Kenyatta, tutazidi kukulilia sisi kama wanawake wa Kerio Valley mpaka usiskie kilio chetu,” alisema Bi Kanda.

“Watu wanauwa kama kuku na serikali inaangalia tu! Kila siku tunazika watoto wachanga wasio na hatia,” mwakilishi maalum huyo aliongezea.

Wezi hao waliovalia sare za polisi wanasemekana kutoroka na kuelekea kaunti jirani ya Baringo.

Viongozi wa kaunti hiyo wametoa wito kwa serikali kuu kuingilia kati na kunusuru wenyeji ambao maisha yao yako katika daraja telezi.

“Tafadhali serikali tusaidie watu wetu wanaumia na hatujui kesho tutaamka vipi, vifo vimejaa kila kona kufikia. Tumezika zaidi ya watu 80 na miongoni mwao ni watoto,” alisema naibu gavana Elgeyo Marakwet Wesley Rotich.

Waliojeruhiwa wanatibiwa katika hospitali kuu ya rufaa ya Moi, Eldoret huku uchunguzi wa kuwasaka wahusika ukiendelea.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *