
Mwanamume kule Mumias aliamuriwa kutembea uchi baada ya kuibia mama mboga Sh 200 [Picha-Hisani]
Kizaaza kilishuhudiwa Ekero, Mumias katika kaunti ya Kakamega, baada ya mshukiwa wa wizi kuvuliwa nguo na kuamrishwa kwenda nyumbani kwake akiwa uchi wa mnyama.
Mshukiwa ni mhudumu wa pikipiki ambaye anatambuliwa kama Juma na anasemekana kuingia katika kibanda cha mama mboga karibu na kituo cha kuegesha magari cha Ekero kununua mboga kabla ya kuchukua Sh 200 za mama huyo.
Mwanabodaboda huyo, ambaye anahudumu katika mji wa Mumias, anasemekana kuchukua hela hizo za Mary Mukhwana wakati mama huyo alikuwa akishughulika kumfungia mboga.
“Ilikuwa mwendo wa saa 1:20 mchana ambapo kijana huyo alikuja kwa kibanda changu kununua mboga ndipo nilipogundua alikuwa akiinua kitambaa ndipo nikagundua alikuwa ameniibia shilingi 200,” Bi. Mukhwana alisema.
Muda mfupi baada kugundua hivyo, Bi Mukhwana alianza kupiga mayowe huku akiwa amemkaba kijana huyo koo, jambo lililowavutia wafanyibiashara wengine.
Umati wa watu ulifurika hapo na kijana huyo alipopekuliwa mfukoni hakika alipatikana na shilingi 200.
Halaiki hiyo ya watu, badala ya kumvamia na kumpiga jinsi ilivyo ada, ulimuamuru atoe nguo abaki uchi wa mnyama mchana peupe na atembee vivyo hivyo mpaka kwake, huku watu wakimcheka.

Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.