Mwanamke mmoja mwenye umri ya miaka 40 kutoka kijiji cha Ujwang katika eneo bunge la Ugenya, Siaya, anauguza majeraha mabaya katika hospitali ya rufaa ya Busia baada ya kukatakatwa vibaya na mumewe kufuatia mzozo wa kinyumbani.
Judith Anyango anadai mumewe Jactone Opondo alimshambulia kwa upanga usiku wa kuamkia Jumanne baada ya wao kutofautiana kimapenzi.
Judith anadai mumewe alikuwa na mpango wa kando, jambo lililopelekea tukio hilo.
Maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi kihusiana na swala hilo na wanamsaka mumewe.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.