Magazeti ya Alhamisi, Machi 31, yameripotia kwa kina uamuzi uliyokuwa ukisubiriwa kwa hamu kuhusu uhalali wa Mpango wa Maridhiano wa BBI ambao utatolewa baadaye leo katika Mahakama ya Upeo.
Magazeti haya pia yameripoti kuhusu sherehe za wanafunzi walioandikisha matokeo mazuri katika mtihani wa KCPE 2021.
- Daily Nation
Gazeti hili linaripoti kuwa Naibu Rais William Ruto alimpa kiongozi wa ODM Raila Odinga na washirika wake ofa ya nusu ya nyadhifa kuu za serikali kama malipo ya kumsaidia kumng’oa Rais Uhuru Kenyatta mamalakani.
Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed aliambia Daily Nation alikuwa sehemu ya kikosi kilichojadili na Ruto mapendekezo ya kumuondoa Uhuru mamlakani.
Katika mazungumzo hayo yaliyoanza mara moja Uhuru alipochaguliwa kwa muhula wa pili mwaka 2017, Junet alifichua kuwa Raila alipewa nafasi ya naibu rais huku Ruto akichukua uongozi wa nchi.
Mbunge huyo alisema Ruto aliwafikia ili wamsaidie kumuondoa Uhuru mamlakani, ambaye alihisi tayari anaonyesha dalili za kumsaliti baada yake (Uhuru) kutangaza kuwa hatagawana mamlaka na yeyote alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa makundi ya wabunge wa Jubilee aliouandaa baada ya uchaguzi.
Junet alisema makubaliano hayo yalikuwa ya kuvutia sana lakini walilazimika kuhoji ni kwa nini Raila angechukua wadhifa wa naibu rais ilhali alikuwa mgombea bora zaidi wakati huo.
Katika njama hiyo, Raila alipaswa kuwakusanya angalau wabunge 100 katika Seneti na Bunge la Kitaifa ili kuongeza kwenye idadi ambayo Ruto angeleta kutoka Jubilee kufikia kiwango cha 234 kinachohitajika kumvua Uhuru madarakani.
Ili ionekane kama ajenda ya upinzani, Junet alisema ODM kilikuwa kiwasilishe hoja ya kumuondoa Uhuru bungeni na wabunge hao wangehongwa kati ya KSh 300,000 na KSh 500,000 kila mmoja.
- The Standard
The Standard linaripoti kuwa huku Mahakama ya Upeo ikitarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu BBI ambayo ilikuwa imependekeza kupanuliwa kwa serikali, macho yote yataelekezwa kwake kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka.
Kalonzo amekuwa kimya tangu alipokaribisha Uhuru na kiongozi wa KANU Gideon Moi nyumbani kwake Karen mnamo Machi 19.
Kwa muda wa wiki mbili, Kalonzo hajakuwa akionekana kwenye hafla za kisiasa wala kuitisha mkutano wowote na wanahabari.
Wakati viongozi wa Azimio la Umoja walipokuwa wakimfanyia kampeni Raila alipokuwa katika ziara yake ya siku tano nchini Uingereza, Kalonzo pia alijikunja.
Duru ziliarifu gazeti hili kwamba Wiper inasemekana kushikilia msimamo wake wa kutodai chochote isipokuwa mgombea mwenza na kwamba muungano wa Azimio-One Kenya awe wao.
- The Star
Gazeti hili linaliripoti kuwa wabunge wamefutilia mbali mapendekezo ya IEBC na kuidhinisha mabadiliko makubwa ya sheria za uchaguzi ambayo sasa yatailazimisha IEBC kuwasilisha moja kwa moja matokeo ya uchaguzi wa urais.
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ilitaka kufutiliwa mbali kwa Kifungu cha 39 (1G) cha Sheria ya Uchaguzi, ambacho kinawalazimisha kupeperusha matokeo moja kwa moja.
Sehemu hiyo ilitangazwa kuwa kinyume na katiba na Mahakama ya Juu katika kesi ya Maina Kiai na IEBC ikitaka ifutwe ili kuzingatia uamuzi wa mahakama.
Hata hivyo, IEBC ilishindwa kupendekeza njia mbadala ya ulinzi ili kuhakikisha makadirio ya wakati halisi ya matokeo kutoka kwa vituo vya kupigia kura.
Kama time ya nguvu ya Haki na Masuala ya Kisheria inayoongozwa na Muturi Kigano ilikataa pendekezo la IEBC la kuondoa kipengele hicho, hivyo basi kutunga sheria ya utiririshaji wa moja kwa moja wa matokeo ya urais.
Discover the pulse of Western Kenya with WKT – your go-to digital media platform for real-time updates, rich perspectives, and powerful stories that matter.