Magazeti ya Ijumaa yameripoti pakubwa kuhusu uamuzi wa mahakama ya Upeo kuhusu mswada wa marekebisho ya Katiba BBI.
Majaji saba wa mahakama hiyo walipiga jeneza la BBI msumari wa mwisho katika kesi iliyoamuliwa Alhamisi Machi 31.
People Daily
Jarida hili limeripoti kuhusu hisia za naibu rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga baada ya Mahakama ya Upeo kutoa uamuzi wake wa kutupa nje BBI.
Raila ameashiria mipango ya kufufua mswada huo aksiema ni lazima Wakenya waliokuwa wakiuunga wapate walichotaka.
“Tutajadiliana kuhusu yale ambayo yametokea na tujue ni lipi tutafanya siku zijazo ili kulinda haki za waliokuwa wamepiga kura ili kuona mageuzi,” Raila alisema.
Kwa upande mwingine, naibu rais alisema kile anasubiri ni Raila na Rais Uhuru Kenyatta kuomba msamaha.
Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.