Wenyeji wa kijiji cha Musembe kilichoko eneo bunge la Lugari, kaunti ya Kakamega, wameachwa vinywa wazi baada ya mwili wa mwanamume wa makamo kupatikana ukielea Mto Kipkaren.
Mwendazake, Solomon Lusemo Sangala, 47, ni mraibu wa pombe na aliondoka nyumbani Alhamisi juma lililopita na juhudi za kumtafuta ziligonga mwamba ndipo baadaye wakaarifiwa kuwa mwili wake umepatikana ukielea juu ya maji. Hii ni kwa mujibu wa familia yake
Akidhibitisha kisa hicho, naibu wa chifu wa eneo hilo Bi Pamela Siangu amesema mwili wa mwendazake ulipatikana na mkulima mmoja ambaye alikuwa akifyeka shamba lake kando kando ya mti huo.
“Kuna mkulima mmoja alikuwa anafyeka shamba lake ndipo alipoona kitu kikielea juu ya maji na aliposonga karibu, akaona ni mwili wa mtu na kwa haraka akaarifu idara husika,”alisema Bi. Siangu.
Wenyeji wanatoa wito kwa idara husika kutegua kitendawaili eneo hili ambapo chini ya wiki moja watu wa wawili wamekufa maji.
Mwili wake uliondolewa na maafisa wa kituo cha polisi cha Lumakanda na unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya Kimbilio iliyoko kaunti jirani ya Uasin Gishu huku uchunguzi kuhusiana na kifo chake ukianzishwa.
- Please take a moment to give feedback to this article:
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.