Magazetini: Kalonzo mbioni kumrithi Raila Azimio

Magazetini: Kalonzo mbioni kumrithi Raila Azimio

Kalonzo anaweka mikakati kushawishi uongozi wa Azimio la Umoja kumvika madaraka anapojitayarisha kusimama urais 2027.

Magazeti ya Jumanne, Januari 3, yameangazia masuala kadhaa yakiwemo mpango wa Kalonzo kumrithi Raila katika Azimio.

1. Daily Nation

Chapisho hili linaripoti kuwa jitihada za kuwapatanisha wanasiasa ambao sasa wametengana, zimezua mgogoro huku baadhi ya washirika wao wakitaja hatua hiyo kama isiyokuwa lazima.

Mpango wa wazee wa Mlima Kenya wanaotaka Naibu Rais Rigathi Gachagua kuongoza mazungumzo hayo sio jaribio la kwanza la kutatua mzozo kati ya wanasiasa hao wawili.

Gazeti hili linaripoti kuwa Kiago alisema mchakato unaendelea na utaanza kwa kuwapatanisha Uhuru na msaidizi wake wa zamanai, DP Gachagua.

Mipango ya wazee hao hata hivyo haujapokelewa vyema huku washirika wa viongozi wao wakieleza kuwa nguvu hiyo inapaswa kuelekezwa katika kukomboa uchumi wa nchi.

2. The Standard

Gazeti hili linaripoti kuwa mvutano wa kuudhibiti muungano wa Azimio la Umoja One Kenya unazidi kupamba moto huku kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka akijiandaa kuchukua jukumu hilo.

Lakini kiongozi huyo wa Wiper hawezi kurithi uongozi wa muungano huo ambao kinara wake Raila Odinga anaungwa mkono na aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta.

Kalonzo amekuwa akiweka mikakati ya kutwaa ngome za kisiasa za Raila huku akipanga kuwania kiti cha urais mwaka wa 2027.

Seneta wa Kitui Enoch Wambua alisema kuwa Azimio iko imara na Kalonzo ndiye anayefaa kuwa mgombeaji urais 2027 kwa kuwa alijitolea kuwaunga mkono Raila na Uhuru.

Seneta huyo alishikilia kuwa hakuna mgogoro katika mrengo wa Azimio na Wiper hakina shida na Raila na Uhuru kusalia katika uongozi wa muungano huo kwa muda watakao.

Lakini Katibu Mkuu wa Jubilee Jeremiah Kioni alisema mjadala wa urithi ulikuwa umeanza mapema.

Alisema kuwa kibarua kikubwa cha Azimio hivi sasa ni kuikosoa serikali na kuhakikisha kuwa gharama za umeme zinapunguzwa, bei za vyakula ni nafuu, uhamisho wa fedha wa Inua Jamii unarejeshwa na kuwepo kwa uwazi kuhusu Mtaala unaozingatia Umahiri

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *