Magazeti ya Jumatano, Januari 4, yameangazia matukio kadhaa ikiwemo mipango ya Rais William Ruto katika mwaka mpya wa 2023.
- The Star
Mwanamke mmoja alikamatwa kuhusiana na kifo cha mwanawe mwenye umri wa miaka 15, katika eneo la Suna Magharibi, Kaunti ya Migori. Polisi wanaamini kuwa mvulana huyo alifariki kutokana na majeraha aliyopata na kichapo cha mamake usiku wa kuamkia mwaka mpya.
Mwanamke huyo alikamatwa Jumanne jioni baada ya majirani kugundua maiti ya mwanawe.
Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Migori, Mark Wanjala, alisema mshukiwa ambaye ni mfanyabiashara huko Migori, aliondoka nyumbani kwake Jumanne asubuhi akiamini kuwa mwanawe ambaye alikuwa mwanafunzi wa Kidato cha Pili katika Shule ya Upili ya Abwao alikuwa amelala kutokana na kichapo alichopata usiku uliopita.
Kulingana na Wanjala, mama huyo alishtuka sana kutambua kifo cha mwanawe ambaye polisi bado hawajabaini chanzo cha kifo chake. Alisema hata hivyo, wanashuku kuwa alifariki dunia kutokana na majeraha kwenye mwili wake. Nia ya kutandikwa kwake bado haijulikani.
Mwili wa marehemu ulikuwa na michubuko michache kwenye magoti yake.
Polisi pia wameanza msako wa kumtafuta kaka yake wa mvulana huyo ambaye pia anadaiwa kushiriki katika tukio la kumpiga mdogo wake.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika hifadhi ya Hospitali ya Migori Level IV kwa uchunguzi wa maiti huku upelelezi ukiendelea.
- The Standard
Gazeti hili linaripoti kuwa Rais William Ruto ameanzisha mipango yake ya mwaka mpya huku akitarajiwa kutatua masuala kadhaa ya kiuchumi na kisiasa.
Zaidi ya yote, anapaswa kufanya miujiza ili kupunguza gharama ya maisha kwa wananchi waliolemewa na sera za kiuchumi za utawala wa Jubilee ambao alikuwa sehemu yake.
Katika upande wa kisiasa, Upinzani unataka kutawala uongozi wake na mgongano wa malengo katika muungano wake wa Kenya Kwanza.
Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.