
Waziri wa Zamani Prof. George Magoha/Courtesy
Aliyekuwa Waziri wa Elimu katika serikali ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, Prof. George Magoha, atazikwa Jumamosi hii nyumbani kwake Gem, kaunti ya Siaya.
Akidhibitisha tamko hilo, naibu rais Rigathi Gachagua, ameihakikishia familia ya Prof. Magoha kuwa serikali itaisadia katika kuandaa mazishi yake.
Gachagua aliongoza Baraza la Mawaziri pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu serikalini katika kuifaraji familia ya Prof. Magoha mtaani Lavington wiki iliyopita ambapo alitoa rambirambi zake rais William Ruto.
Ruto alimtaja mwendazake kuwa mtu aliyejitoa mhanga kazini kuhudumia umma.
“Serikali itatoa ndege ya jeshi la wanahewa kusafirisha mwili wa mwendazake,” alisema naibu huyo wa rais.
Magoha aliaga wiki moja iliyopita kwa kile madaktari wa hospitali kuu ya Nairobi walisema ni mshutuko wa moyo.

Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.