
Mchezaji wa timu ya taifa ya Morocco na klabu ya PSG, Achraf Hakimi/Hisani
Nyota wa Paris Saint-Germain (PSG) na timu ya taifa ya Morocco Achraf Hakimi raia ameshtakiwa kwa ubakaji baada ya kudaiwa kumwalika mwanamke nyumbani kwake wakati mkewe na watoto wake wakiwa likizo.
Mshtaki wake anadai kuwa baada ya kufika nyumbani kwake, nyota huyo wa mpira wa miguu alianza kumbusu mdomoni huku akinyanyua nguo zake.
Alidai alimbusu kwenye matiti yake licha ya kumpinga kabla ya kumuingilia kimwili bila ridhaa yake. Hii ni kulingana na jarida la The Sun.
Kwa sasa, maafisa wa polisi wa taifa la Ufaranza wameanzisha uchunguzi kuhusiana na madai hayo.

Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.