Magazeti ya Jumanne, Aprili 4, yameangizia hali ya kisiasa nchini kufuatia makubaliano kati ya rais William Ruto na kiongozi wa Azimio Raila Odinga.
People Daily
Chapisho hili linaripoti kuwa japo Ruto na Raila walikuwa wakiwasiliana wikendi, wawili hao hawakuwahi kukutana uso kwa uso.
Wawili hao waliwasiliana kupitia kwa afisa mkuu katika Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma (ODPP) ambaye alikuwa akituma na kupeleka ujumbe kutoka kwa chama kimoja hadi kingine.
Duru zilidai kwamba rais alikataa pendekezo la viongozi wa kidini ambao walikuwa wakishinikiza akutane na Raila moja kwa moja.
Kutokana na kukosekana kwa mazungumzo ya moja kwa moja, afisa mkuu serikalini ndiye alitumika kuwasilisha misimamo ya viongozi hao wawili.
Mazungumzo hayo yalikuwa siri kubwa sana na ni watu watatu tu kutoka upande wa rais Ruto ndiyo waliofahamu yaliyokuwa yakiendelea ambao ni Waziri wa Usalama Kithure Kindiki, mwenzake wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen na Seneta wa Kericho Aaron Cheruiyot.
Kwa upande wa Raila, ni mgombea mwenza wake pekee katika kinyang’anyiro cha urais 2022, Martha Karua, na kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ndiyo walijua.
Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Eugene Wamalwa, kiongozi wa Chama cha Roots George Wajackoya na viongozi wengine wa Azimio waliwekwa gizani hadi dakika ya mwisho.
Viongozi wa kidini waliwaendea viongozi hao wawili moja kwa moja baada ya kugundua kuwa mazungumzo hayo yalikuwa yakitatizwa na na watu wenye msimamo mkali katika pande zote.
Kutokana na hali hiyo, wapatanishi hao waliwataka viongozi hao wawili kuwaacha nje washirika wao waliodhaniwa kuwa vizingiti katika kuwapatanisha.
Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.