Staa wa Manchester United Marcus Rashford amevunja kimya chake baada ya kichapo cha haja mikononi mwa Liverpool ugani Anfield Jumapili.
The Red Devils walitoa kimyani mabao saba bila jibu katika ngaramba iliyofichua ulegevu katika kikosi cha mkufunzi matata Eric Ten Hag.
Rashford anakiri ukosefu wa umakinifu katika mechi hiyo na ameomba umoja kambini.
“Natamani tungecheza mechi nyingine leo ili tulainishe maneno. Matokeo ni matokeo na hatuwezi tazama zaidi ya hapo! Hili haliwezi kutathmini mwelekeo wetu msimu huu. Lazima tuamini uwezo wetu na tusalie kama timu moja,” alisema kupitia ukurasa wake katika mtandao wa Twitter.
Kipigo cha Liverpool ndio kikubwa zaidi kwa Manchester United na kinaendeleza ubabe wa wapinzani wao hususan wanapokutana Anfield.
The Red Devils wameshinda mechi tatu tu Anfield, ya mwisho ikiwa mnamo January 2016.
Thanks for choosing WKT. Advertise with us for affordable offers.