Mamake winga wa zamani wa Nairobi City Stars, David Agesa, anawaomba wadau wa soka kumsaidia mwanawe kurejea nchini baada ya mkataba wake wa uhamisho wa kwenda Malaysia kuporomoka.
Akizungumza na kituo kimoja humu nchini, Linet Shirinji, mamake mchezaji huyo, alisema mwanawe alikwenda Malaysia mwezi Mei kwa ajili ya kuandikisha mkataba na wakala wake, raia wa Ivory Coast.
Wakala huyo alimuarifu kuwa mkataba haujakuwa tayari kabla ya kumuacha akikwama bila timu ya kuchezea.
“Tunahangaika tu, namtumia kitu kidogo ninachopata ili ajisimamie. Mimi mwenyewe sina pesa,” alisema mamake Agesa.
Visa ya kukaa katika taifa hilo la Kusini Mashariki mwa Asia imepita na gharama ya kumkimu katika nchi hiyo ya kigeni imekuwa mzigo kwa mamake.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.