Kurt Zouma wa West Ham mashakani kwa kumnyanyasa paka wake
Mchezaji Kurt Zouma wa West Ham [Picha-Getty Images]

Kurt Zouma wa West Ham mashakani kwa kumnyanyasa paka wake

Beki wa klabu ya West Ham United na timu ya taifa ya Ufaranza, Kurt Zouma, anaweza kufunguliwa mashtaka baada ya kurekodiwa kwenye video akimpiga paka wake kama ngoma.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 pia anaonekana akimpiga usoni paka huyo.

Klabu yake imelaani kitendo hicho na kusema kuwa itashughulikia swala hilo.

Katika video, beki huyo anaonekana akimshambulia mnyama huyo kwenye jumba lake la kifahari kwa kumpiga teke kisha kumkimbiza mnyama huyo akizungunguka chumba chake cha maakuli mbele ya mtoto huku kaka yake akichukua video akicheka.

Katika video ya mwisho, anaonekana akimpiga paka kwa nguvu usoni.

Jana usiku, Zouma aliomba msamaha kwa tukio hilo.

“Nataka kuomba radhi kwa vitendo vyangu. Hakuna visingizio kwa tabia yangu ambayo ninaijutia sana,” Zouma alikiri.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *