UCL: Miamba wa Ulaya PSG na Real Madrid kumenyana usiku
[Picha-Getty Images]

UCL: Miamba wa Ulaya PSG na Real Madrid kumenyana usiku

Kombe la klabu bingwa barani Ulaya (UCL) linarejelewa rasmi leo usiku huku miamba wa Ufaranza, Paris Saint Germain (PSG), wakikutana leo saa tano usiku katika mechi za raundi ya 16 na vigogo wa Uhispania, Real Madrid.

Ni mechi ambayo imetajwa na wadadisi kuwa ngumu sana.

Timu hizi mbili hazijakutana mara nyingi sana. Mara ya mwisho zilichuana msimu wa 2017/18 ambapo Madrid walishinda 5-2 kwa ujumla.

Leo hii vijana wake Pochettino, PSG, wanatarajia kulipiza kisasi ikizingatiwa wako nyumbani leo na katika hali nzuri sawia na vijana wa Carlo Ancelotti, Real Madrid.

Kwingineko, vigogo wa Uingereza Manchester City wanasafiri nyumbani kwa Sporting CP ya Ureno leo saa tano usiku.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *