Mabingwa watetezi wa Champions League, Chelsea, leo usiku saa 23:00 watajibwaga uwanjani dhidi ya Lille ya Ufaranza katika hatua ya kutetea taji lao katika raundi ya 16.
The Blues wanaingia katika mechi hiyo wakiwa na tabasamu baada ya kupata ushindi wa 1-0 katika EPL wikendi dhidi ya Crystal Palace.
Lille nao wanacheza mchwano huu baada ya kuambulia sare ya 0-0 dhidi ya Metz katika ligi kuu ya Ufaranza.
Katika mechi mbili ambazo Lille wamekutana na Chelsea, hawajapata ushindi wowote.
Chelsea wanashikilia nafasi ya tatu katika ligi kuu ya Uingereza huku Lille wakiwa nambari ya 11 katika ligi kuu ya Ufaranza.
Kwingineko, Villarreal ya Uhispania wanwaalika Juventus wa Italia saa 23:00.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.