Mrusi na mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich, ameondolewa rasmi katika orodha ya wamiliki katika ligi kuu ya Uingereza, hili limedhibitishwa na waandalizi na waendeshaji wa ligi hiyo.
Bwanyenye huyo ameondolewa kwa madai ya kuwa na uhusiano wa karibu na rais wa Urusi, Vladimir Putin, ambaye nchi yake imewekwa vikwazo vya kiuchumi baada ya kuivamia Ukraine kijeshi.
Mali yote ya Abramovich kwa sasa ipo chini ya serikali ya Uingereza.
Kulingana na vikwazo vipya, Chelsea itaendeshwa chini ya leseni maalum huku mfumo wa mishahara ukiwa unafadhiliwa.
Hakuna uhamisho wa wachezajj wapya au mikataba mipya inaruhisiwa kwa sasa sawa na mauzo ya bidhaa.
Duka la klabu hiyo pia limefungwa na hairuhusiwi kuuza tiketi mpya, Badala yake, wale walionunua tiketi za msimu mzima ndio wanaweza kwenda uwanjani wakati The Blues inacheza
Chelsea pia haitakuwa na mashabiki wa ugenini siku zijazo.
Abramovich amezuiliwa kuuza Chelsea FC na mali yake yote iko chini ya serikali ya Uingereza. Hii ina maan kuwa iwapo Chelsea itauzwa, fedha hazitakwenda kwa namna yoyote kwa Mrusi huyo.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.