Mchezaji wa Sheffield ajeruhiwa na shabiki mwenye hasira
Nahodha wa Sheffield United Billy Sharp [Picha-Hisani]

Mchezaji wa Sheffield ajeruhiwa na shabiki mwenye hasira

Mashabiki waliingia uwanjani baada ya Sheffield kupotea dhidi ya Forest.

Nahodha wa Sheffield United, Billy Sharp, aliachwa na majeraha baada ya kushambuliwa na mashabiki kufuatia mchuano wa kufuzu katika daraja ya ligi kuu Uingereza mkondo wa pili dhidi ya Nottingham Forest.

Forest walishinda mchuano huo wa raundi ya pili katika mikiki ya penalti na kughadhabisha mashabiki wa Sheffield ambao waliingia uwanjani baada ya kuona upande wao umelemewa.

Mashabiki walijaa uwanjani baada ya mechi kati ya Sheffield United na Nottingham Forest [Picha-Hisani]

Meneja wa Sheffield United, Paul Heckingbottom, alisema baada ya mechi hapo ndipo Sharp alipojeruhiwa.

“Ni unyanyasaji,”alisema Hecklingbottom. “Tumeona mmoja wa wachezaji wetu akivamiwa. Alibebwa juu, alivuja damu, hasira. Itashughulikiwa.”

Akiwa amesimama tisti, Sharp alivamiwa na shabiki aliyekuwa uwanjani. Sharp alilamba sakafu huku shabiki huyo akitoroka.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 36 ametoa maoni yake katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

“Shabiki mmoja mpumbavu alivuruga kandanda ya usiku huo. Hongera kwa Nottingham Forest kwa ushindi wao na kila la heri katika fainali,” alisema kwa gadhabu.

Share this article
Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *