Mwelekeo wa ubingwa wa Premier League msimu wa 2021/22 utajulikana hii leo katika mechi za mwisho za Liverpool na Manchester City.
Katika msimamo wa jedwali la ligi, Manchester City inaongoza kwa alama 90 huku Liverpool ikifuata kwa karibu kwa alama 89.
Fahali hawa wawili wamecheza mechi 37 kila mmoja.
Katika mechi za kuamua bingwa, Liverpool watamkaribisha Wolves ugani Anfield huku Manchester City wakiwa wenyeji wa Aston Villa ugani Etihad.
Ngaramba mbili hizi zote zitapigwa saa kumi na mbili jioni.
Je, City wanasimama nafasi gani kushinda mechi ya leo?
Manchester City, chini ya mkufunzi wa sasa Pep Guardiola, ina uwezo wa kushinda mechi yao ya mwisho kwa asilimia 84, sare asilimia 11 na kushindwa asilimia 6. Liverpool nayo ina asilimia 82 kushinda, sare asilimia 12 na kushindwa asilimia 6.
The Cityzens wameshinda mechi 9 kati ya 10 za mwisho katika ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Aston Villa. Wameandikisha sare moja ikiwemo mechi sita za mwisho zikifuatana.
Mabingwa hao watetezi walipoteza mchuano wao kwa Aston Villa uwanjani Villa Park Septemba 2013 (2-3).
Aston Villa imepoteza mechi 15 kati ya 16 za mwisho za Ugenini dhidi ya Manchester City huku wakipoteza kila moja kwa mechi 11 kwenye msururu huo tangu washinde 2-0 mnamo April, 2007.
Je, Liverpool wana uwezo gani wa kushinda leo?
Liverpool, ambayo kwa sasa iko chini ya nahodha Jurgel Klopp, imeshinda mechi zote 10 dhidi ya Wolves tangu ipigwe na mbwa mwitu hao 1-0 Anfield Disemba 2010 chini ya uongozi wa Roy Hodgson. Wolves imepoteza mara 17 katika mechi 19 za ugenini dhidi ya Liverpool, na kushinda mechi mbili pekee.
The Reds hawajapigwa mechi zao 6 za EPL za kufunga msimu.
Wolves wamepoteza mechi yao ya mwisho kati ya 6 za ligi 7 ya Uingereza. Hakuna timu sasa hivi ambayo ina kiwango cha chini sana cha kushinda kuliko Wolves (14%).
Iwapo Manchester City itatoka sare ama kupoteza mechi yake dhidi ya Aston Villa na kisha Liverpool ishinde mechi yake dhidi ya Wolves, basi the Reds watabeba kombe.
Discover the pulse of Western Kenya with WKT – your go-to digital media platform for real-time updates, rich perspectives, and powerful stories that matter.