
Ukrasa wa mbele wa Daily Nation/Hisani
Magazeti ya Jumanne, Machi 28, yanaripoti kwa kina kuhusu uvamizi katika shamba la rais mstaafu Uhuru Kenyatta la Northlands na kampuni ya kutengeneza gesi ya Spectre inayomilikiwa na kinara wa Azimio Raila Odinga.
Daily Nation
Mnamo Jumatatu, Machi 27, 2023, makumi ya wahuni walivamia shamba linalomilikiwa na familia ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta katika eneo la Kamakis kwenye barabara kuu ya pembeni ya Eastern Bypass, Nairobi, na kupora mali ya thamani isiyojulikana.
Uvamizi sawia ulifanyika katika kampuni ya kutengeneza mitungi ya gesi ya Specter East Africa, kampuni ambayo inahusishwa na familia ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga anayeongoza maandamano dhidi ya serikali.
Uvamizi huo umehusishwa na kiongozi wa wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah ambaye mnamo Machi 18, 2023, alidokeza kuhusu uvamizi katika mali ya familia ya Kenyatta akimshutumu Uhuru kwa kufadhili maandamano ya Azimio La Umoja One Kenya.
The Standard

Wakati maandamano ya Azimio dhidi ya serikali yalipozinduliwa, iliibuka kuwa tayari mawaziri wasaidizi 50 walikuwa tayari wameapishwa na wengine kuanza majukumu yao mapya.
Haya yalijiri licha ya Mahakama Kuu kukataa kusitisha amri hiyo, huku Jaji Hedwig Ong’udi akiagiza kwamba kesi ya wakili Adrian Kamotho ya kutaka kuondoa maagizo hayo itolewe kwa Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK) na Taasisi ya Katiba ili wapewe nafasi ya kujibu kabla ya kutoa mwelekeo.
Wiki iliyopita, Jaji Ong’udi aliwazuia mawaziri wasaidizi kupokea mishahara au marupurupu hadi kesi iliyowasilishwa na LSK na Taasisi ya Katiba kupinga uhalali wa nyadhifa zao itapoamuliwa.

Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.