Kwenye mahojiano ya hivi karibuni, raia wa Ufaranza na kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba amesema anapambana sana Old Trafford kwa sababu timu hiyo imekosa mfumo maalum wa kucheza.
Mfaranza huyo alisema kuwa anataka kurejesha muda wake wa miaka mitano ambao anasema amepotezea akichezea Red Devils na kukosa mataji wakati mkataba wake utakapomalizika.
“Ni vigumu kuwa kucheza vyema katika kikosi cha Manchester United huku ukibadilishiwa nafasi kila mara, mfumo wa kucheza,” alisema.
Pogba pia amefunguka kuhusu jinsi amekuwa akipambana na msongo wa mawazo na jinsi hali hiyo ilimfanya ajitenge.
“Nimekuwa na msongo wa mawazo katika taaluma yangu na huwa sisemi. Wakati mwingine hujijui wewe ni nani, unataka tu ujitenge, uwe peke yako na ni hatari sana,” alisema Mfaranza huyo.
Pogba ameongezea kuwa kuna haja wa wachezaji wa soka kushirikishwa katika mazungumzo kuhusu afya ya kiakili.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.